WANASAYANSI WAVUMBUA KITAMBAA CHA AINA MPYA KINACHOWAFANYA WATU KUHISI BARIDI ZAIDI



Kikundi cha Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani kimevumbua kitambaa kinachoweza kurudisha mwanga wa jua na kupitisha joto la mwili kwa ufanisi mkubwa. Mtu akivaa nguo iliyoshonwa kwa kitambaa hiki, atahisi baridi zaidi.
Naibu prof. Cui Yi wa idara ya sayansi ya malighafi na uhandisi ya Chuo Kikuu cha Stanford anayeongoza utafiti huo alifahamisha kuwa, malighafi ya kitambaa hiki ni Polyethylene yenye matundu mengi madogomadogo yenye kipenyo cha nanomita kadhaa. Kabla ya hapo, malighafi hii ilitumiwa katika uzalishaji wa betri za Li-ion. Joto la mwili wa binadamu linatolewa kwa njia ya mwanga wa infrared, na malighafi hii inaweza kupitisha mwanga wa infrared bila vizuizi vyovyote. Aidha, matundu madogomadogo yanasaidia kupitisha hewa na unyevu.

Majaribio yanaonesha kuwa mtu akivaa nguo iliyoshonwa kwa kitambaa hiki, joto la mwili wake litaongezeka kwa nyuzi 0.8 tu, lakini akivaa nguo ya kitambaa cha pamba, joto litaongezeka kwa nyuzi 3.5, na akivaa nguo ya kitambaa cha Polyethylene ya kawaida, joto litaongezeka kwa 2.9. Hii inamaanisha kuwa mtu anayevaa kitambaa cha aina mpya atahisi baridi zaidi kuliko vitambaa vingne.

Prof. Cui Yi alisema malighafi hii inatazamiwa kutumiwa kwa wingi katika utengenezaji wa nguo, hasa nguo za michezo, na kikundi chake kitaendelea kutafiti na kuvumbua kitambaa chenye ubora zaidi.
WANASAYANSI WAVUMBUA KITAMBAA CHA AINA MPYA KINACHOWAFANYA WATU KUHISI BARIDI ZAIDI WANASAYANSI WAVUMBUA KITAMBAA CHA AINA MPYA KINACHOWAFANYA WATU KUHISI BARIDI ZAIDI Reviewed by Elimutehama on 00:59:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.