MWANASAYANSI WA KIJAPANI ASHINDA TUZO YA NOBELI YA TIBA


Yoshinori Ohsumi kutoka Japan ndiye mshindi wa tuzo ya nobeli ya tiba ya mwaka huu

Mwanasayansi Yoshinori Ohsumi kutoka Japan ametunukiwa tuzo ya nobeli ya tiba ya mwaka 2016 kwenye hafla iliyoandaliwa katika mji mkuu wa Stockholm nchini Uswidi.
Yoshinori Ohsumi alishinda tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa aliotoa kwenye utafiti wa kisayansi kuhusu muundo wa seli.

Wakati huo huo, Yoshinori Ohsumi pia alituzwa kitita cha fedha takriban dola milioni 1.
Tuzo ya nobeli ya tiba ya mwaka jana ilitolewa kwa wanasayansi 3 waliofanya utafiti wa vimelea na maradhi ya Malaria. Wanasayansi hao ambao ni William Campbell kutoka Ireland, Satoshi Omura kutoka Japan pamoja na Youyou Tu kutoka China walivumbua dawa ya tiba dhidi ya maradhi ya vimelea na Malaria.

Mshindi wa tuzo ya nobeli ya amani naye atatangazwa tarehe 7 Oktoba.
Washindi wote wa tuzo za nobeli watajumuika pamoja tarehe 10 Desemba na kukabidhiwa tuzo zao kwenye hafla rasmi. Kila mwaka tuzo za nobeli hutolewa tarehe 10 Desemba kama desturi ya kumbukumbu ya tarehe ya mwanzilishi wake Alfred Nobel.
MWANASAYANSI WA KIJAPANI ASHINDA TUZO YA NOBELI YA TIBA MWANASAYANSI WA KIJAPANI ASHINDA TUZO YA NOBELI YA TIBA Reviewed by Elimutehama on 01:35:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.