PANASONIC YATENGEZA BETRI INAYOJIPINDA

Vifaa vinavyojipinda katika soko huenda vikawa vingi kufuatia hatua ya kampuni ya Panasonic kuvumbua betri ya lithium inayoweza kujipinda katika maonyesho ya kiteknolojia nchini Japan.

Betri hiyo inaweza kutumika katika saa,bangili na nguo.Ni ndogo ,ikimaanisha haiwezi kutumika katika simu aina ya smartphone katika awamu hiyo.

Wataalam wanasema kuwa ni uvumbuzi mzuri ,ijapokuwa Panasonic sio kampuni ya kwanza kutengeza betri hizo. Ben Wood ambaye ni mchanganuzi wa kampuni moja ya utafiti CCS ameaimbia BBC:Watengenezaji wengine kama vile LG na Samsung pia wameanzisha juhudi za kutengeza vifaa vinavyoweza kujipinda ,kama vile betri na vioo.
PANASONIC YATENGEZA BETRI INAYOJIPINDA PANASONIC YATENGEZA BETRI INAYOJIPINDA Reviewed by Elimutehama on 01:32:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.