KODI YA PANGO LA ARDHI KULIPWA KIELEKTRONIKI
Serikali kupitia Wizara Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi imefanikiwa kuandaa mfumo mpya wa kielektoroniki wa ukusanyaji wa maduhuri ya serikali ambayo ni kodi ya pango la ardhi mfumo ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya makusanyo ya kodi.Unaolenga kupunguza kero wanazopata walipa kodi ya kutumia muda na mlolongo mrefu wakati wa kulipia.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Denis Masami amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba mfumo huo wa kulipia kodi kwa njia ya Mtandao unatumia njia tatu za kukadiria na kulipia kodi ambazo ni njia ya Tovuti ya Wizara, kwa kutumia simu yake ya mkononi au kulipia kupitia benki, pamoja na njia ya dawati la makadirio ya Kodi lililoko Wizarani utasaidia kuondoa udanganyifu wa malipo ya pango la ardhi ambao umekuwa ukilalamikiwa na wamiliki wengi wa kodi ya pango la ardhi ukihusishwa na madai ya kuwepo vitendo ya rushwa .
Pamoja na hayo, wizara hiyo imepanga kushirikiana na serikali za mitaa kufanya ukaguzi maalumu wa maeneo yote ya ardhi yasiyopimwa, ili kujua ni wananchi wangapi wana maeneo hayo na maeneo gani, waweze kuingizwa kwenye mfumo wa kulipia kodi ya ardhi.
Aliwatahadharisha wale wote wanaomiliki ardhi na kuwa na hati au ofa, kuhakikisha wanalipia kodi hiyo kwa wakati, vinginevyo muda wa malipo ukipita watatozwa faini na wasipolipa pia baada ya siku 14 wataburuzwa mahakamani. Kwa mujibu wa mfumo huo, wanaotumia mitandao ya simu wanatakiwa kupiga namba *152*00# na kufuata maelekezo, na kwa wale wanaotumia mtandao wa wizara waingie kwenye tovuti www.ardhi.go.tz.
KODI YA PANGO LA ARDHI KULIPWA KIELEKTRONIKI
Reviewed by Elimutehama
on
23:20:00
Rating:
No comments: