MAREKANI YACHUNGUZA SHAMBULIO KUBWA LA MTANDAO



Mamlaka nchini Marekani imesema inachunguza shambulio kubwa la kimtandao ambalo limekumba mifumo ya kompyuta duniani kote.
Baraza la Taifa la Usalama jijini Washington limesema Marekani imedhamiria kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.
Mashirika mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha, idara za serikali, makampuni makubwa, na kampuni za usafirishaji ni miongoni mwa zilizoathirika.

Watumiaji wameambiwa komputa zao zimenasa mpaka walipe kiasi cha dola mia tatu katika akaunti isiyofahamika. Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imewashauri watu wasilipe fedha hizo.
Huku ikisema hakuna uhakika kwamba, mafaili yaliyofungwa yatafunguka baada ya malipo hayo kufanyika. Shambulio hilo la kimtandao lilianza nchini Ukraine na linaendelea sehemu nyengine duniani.

chanzo:bbc
MAREKANI YACHUNGUZA SHAMBULIO KUBWA LA MTANDAO MAREKANI YACHUNGUZA SHAMBULIO KUBWA LA MTANDAO Reviewed by Elimutehama on 00:40:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.