SIDIRIA INAYOWEZA KUGUNDUA SARATANI YA MATITI



Kijana mmoja nchini Mexico amevumbua sidiria inayoweza kugundua saratani ya matiti. Lakini je sidiria hiyo inafanya kazi? Na iwapo inafanya ,inafanya vipi?. Juliana Rios Cantu mwenye umri wa miaka 18 ametengeza sidiria ambayo anasema itatoa onyo la mapema kwa mtu mwenye dalili za saratani hiyo.
Sidiria hiyo kwa jina Eva iliotengezwa naye na marafikize watatu walianzisha kampuni hiyo pamoja. Lakini wamechangisha fedha ili kuifanyia majaribio na wiki hii wakashinda tuzo katika hafla ya wanafunzi wanaotaka kufanya biashara.

Kampuni yao Higia Technologies iliibuka mshindi baada ya kuzishinda kampuni nyengine za biashara kutoka kote duniani ili kushinda dola 20,000 kuzalisha wazo lao. Wazo la sidiria ya Eva ni kwamba ina sensa ambazo inaweza kupima viwango vya joto, kuviweka katika programu na kumuelezea kuhusu mabadiliko yanayomsumbua.
Wanawake wanaohitaji sidiria hiyo watalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki ili kupata vipimo vya sawa. Hii ni awamu ya kwanza ya dalili za ugonjwa huo. Tayari sidiria hiyo imefanyiwa majaribio na itafanyiwa vipimo vyengine vya kimatibabu kabla ya wataalam wa ugonjwa wa saratani kuipendekeza kuwa njia ya kugundua saratani.
SIDIRIA INAYOWEZA KUGUNDUA SARATANI YA MATITI SIDIRIA INAYOWEZA KUGUNDUA SARATANI YA MATITI Reviewed by Elimutehama on 05:53:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.