NDEGE KUBWA AINA YA C919 YASAFIRI KWA MARA YA KWANZA



Ndege kubwa aina ya C919 inayotengenezwa na China leo imefanya safari ya kwanza kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pudong wa Shanghai.
Kwa mujibu wa mpango, safari hiyo ya kwanza ya C919 imechukua muda wa dakika 90. Ndege ya aina hiyo yenye viti 168 inatengenezwa na China kwa kufuata kwa makini viwango vya kimataifa, na pia inaongoza aina nyingine za ndege za kiwango hicho katika pande nyingi. Naibu msanifu mkuu wa ndege hiyo Bw. Zhou Guirong anasema:
"Mfumo wa umeme wa C919 una uwezo mkubwa zaidi ikilinganisha na aina nyingine za ndege za kiwango kama hicho, kwani tumetumia muundo mpya ambao unaweza kuboreshwa kwa njia ya Software, tena gharama za uboreshaji ni za chini."

Bw. Zhou Guirong ameeleza kuwa, C919 imekusanya aina nyingi za uwezo mpya katika sekta hiyo, zikiwa ni pamoja na sensa (sensor) mpya inayoweza kuhakikisha usalama wa ndege wakati wa hali mbaya ya hewa, na kutumia teknolojia ya Wireless broadband system ili kuwawezesha abiria kufanya mawasiliano na ardhini wakati wanasafiri angani.

Ndege aina ya C919 ni ndege kubwa ya kwanza ya abiria iliyosanifiwa na kutengenezwa na China. Mhandisi mkuu wa upashanaji wa habari wa ndege hiyo Bw. Pan Lingyun ameeleza kuwa, utengenezaji wa ndege za abiria umetumia muundo wa kisasa wa uzalishaji, teknolojia na vifaa, pia imepata maendeleo kwa kasi katika sekta ya utengenezaji wa kidigitali. Anasema: "Teknolojia hizo zinaleta ufanisi mkubwa, na kusaidia sana katika kupunguza gharama za utafiti na utengenezaji."

Imefahamika kuwa, baada ya safari hiyo ya kwanza, kazi ya utafiti na utengenezaji wa C919 itaanza katika kipindi kipya. Katika siku za baadae, ndege 6 za aina hiyo zitatengenezwa kwa ajili ya kufanyiwa majaribio mbalimbali, ili kuharakisha mchakato wa utafiti na utengenezaji wa rasmi wa ndege hiyo. Katika kipindi kijacho, C919 itaingia katika kipindi cha kufanyiwa ukaguzi. Baada ya kupewa kibali cha kusafiri, itaingia katika uendeshaji wa soko. Hivi sasa ndege ya aina hiyo ina wenzi 23 wa ushirikiano wa nchini na nje ya China zikiwa ni pamoja na Air China, na Kampuni ya GE ya Marekani. Naibu msanifu mkuu wa C919 Bw. Fu Guohua anasema:

"China ina mahitaji makubwa ya ndege mpya, katika siku za baadaye, kadiri uchumi wa China utakavyoendelezwa, hususan sekta ya ugavi wa bidhaa, inakadiriwa ndege 2000 zitahitajika."
Ndege aina ya C919 ni ndege kubwa iliyotengenezwa kushindana na Airbus 320 pamoja Boeing 737.
NDEGE KUBWA AINA YA C919 YASAFIRI KWA MARA YA KWANZA NDEGE KUBWA AINA YA C919 YASAFIRI KWA MARA YA KWANZA Reviewed by Elimutehama on 05:58:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.