SHAMBULIZI LA MITANDAO LAATHIRI MATAIFA 150.
Kirusi cha kompyuta kijulikanacho kwa jina la "ransomware" kimeathiri mitandao ya nchi 150. Kwa mujibu wa habari,kirusi hicho ambacho kilitabiriwa kuisha siku ya Jumatatu kina uwezekano wa kufanya hitilafu kwa mara nyingine.
Katika mazungumzo yake Wainwright na kituo cha ITV,inaonekana kuwa mashirika makubwa na sehemu nyingi za kufanyia kazi zimepata athara kubwa kutokana na kirusi hicho.
Hata hivyo bwana Wright amesema kuwa kuna uwezekano wa tatizo hilo kuongezeka baada ya watu kurejea makazini siku ya Jumatatu.
Ripoti zinaonyesha kuwa huenda shambulizi hilo la mitandaoni likawa la kihalifu. Kirusi cha kompyuta cha "Wannacry" kimeathiri zaidi ya nchi 90.
SHAMBULIZI LA MITANDAO LAATHIRI MATAIFA 150.
Reviewed by Elimutehama
on
09:19:00
Rating:
No comments: