ROBOTI MPISHI AMBAYE ANAWEZA KUPIKA MLO WOWOTE NA KUSAFISHA BAADA YA KUPIKA.



Fikiria roboti mpishi kwamba anaweza kukupikia chakula chochote unachokitaka na kisha anafanya kazi ya kuosha vyombo pia.
Kampuni ya Moley inatarajia kutoa roboti ambayo inafanya kazi hii katika mwaka 2018, na itakuwa na uwezo wa kufikia ukomo kwa mpishi na maelekezo yao duniani kote. Kwenye tovuti yao, walisema: "Hebu fikiria sahani kutoka Michelin-moja ya migahawa ya juu, kupikwa na Mpishi mkuu mbele yenu, katika jiko lako mwenyewe, wakati wowote unapotaka."

Wanadai ni ya kwanza duniani " ni ya kwanza yenye ukamikamilifu na kujumuishia akili ya kupiki kwa roboti". Inauwezo wa kujifunza jinsi ya kupika mapishi yoyote na inaweza kusafisha baada ya kupika yenyewe. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Moley , Mark Oleynik, unaweza kutaja idadi ya watu waliopo, aina ya vyakula, kuhesabu aina ya lishe , viungo taka, mbinu ya kupikia, na mpishi, kupima viungo na kisha inanza kupika.baadaye inaosha vyombo vyote baada ya wewe kula.



Mashine ina vyombo vyote muhimu, na vifaa vya kupika – wewe unachohitaji kumuwekea viungo tu apike. Watumiaji watakuwa na uwezo wa kuchagua orodha ya chakula hata wakiwa mbali na kurudi nyumbani mlo ukiwa tayari kupikwa.Mashine kwa sasa inajua mapishi ya aina mia moja.

Jaribio likionyesha jiko la Moley linaweza kupika mapishi yoyote kwenye mtandao. Pia unaweza kufanya kazi jikoni pia kwa kutumia jiko hilo wakati roboti imezimwa.

ROBOTI MPISHI AMBAYE ANAWEZA KUPIKA MLO WOWOTE NA KUSAFISHA BAADA YA KUPIKA. ROBOTI MPISHI AMBAYE ANAWEZA KUPIKA MLO WOWOTE NA KUSAFISHA  BAADA YA KUPIKA. Reviewed by Elimutehama on 02:28:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.