UBER WAPELEKWA MAHAKAMANI KWA KUIBA SIRI ZA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA KUJIENDESHA MAGARI BINAFSI KUTOKA GOOGLE



Waymo, ni kampuni iliyoanzishwa na Google kutoka umiliki wa Alphabet, imechukua hatua za kisheria dhidi Otto, kitengo cha Uber cha magari ya binafsi ya kujiendesha , kitengo ambacho kilinunuliwa mwaka jana kwa dola $ 700milioni.Kesi hiyo inasema kuwa meneja wa zamani Waymo Anthony Levandowski alichukua habari wakati alipoondoka kwa na kuanzisha kampuni au mradi aliouita Otto.
Waymo ilifungua mashitaka dhidi ya Uber Alhamisi, kwa madai ya njama za pamoja katika kuiba siri ya biashara yake na haki miliki. Kesi hiyo ipo katika Mahakama ya Wilaya California.

Waymo inadai kuwa mfanyakazi wake wa zamani Anthony Levandowski alipakuwa maelfu ya faili za siri kwa teknolojia ya magari binafsi kwa bidii kabla ya kujiuzulu kutoka katika kampuni. Levandowski kisha akazindua kampuni yake binafsi ya magari yanayojiendesha na kuita, Otto, ambayo Uber walinunua mwaka 2016. Waymo pia ina madai kwamba wafanyakazi wengine wao wa zamani ambao wapo Uber pia walipakuwa taarifa za siri.

"Tuligundua kuwa wiki sita kabla ya kujiuzulu kwake mfanyakazi huyu wa zamani, Anthony Levandowski, alipakuwa zaidi ya faili 14,000, mafaili yaliyopakuliwa yanakadiriwa kuwa na ukubwa wa 9.7GB ambayo ni mafaili yenye siri za Waymo zenye kuonyesha vifaa mbalimbali na siri za biashara, ikiwa ni pamoja na mikataba, faili za kubuni na za majaribio." Google ilisema."
UBER WAPELEKWA MAHAKAMANI KWA KUIBA SIRI ZA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA KUJIENDESHA MAGARI BINAFSI KUTOKA GOOGLE UBER WAPELEKWA MAHAKAMANI KWA KUIBA SIRI ZA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA KUJIENDESHA MAGARI BINAFSI  KUTOKA GOOGLE Reviewed by Elimutehama on 04:26:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.