ROBOTI KUPOKEA WAGENI HOSPITALINI UBELGIJI



Roboti kwa jina Pepper, iliyotengenezwa kuelewa hisia za watu inatarajiwa kuanza kazi mpya kama karani wa mapokezi katika hospitali mbili nchini Ubelgiji.

Roboti hiyo itakuwa ya kwanza kuhudumu katika jumba la matibabu baada ya roboti nyengine kuwekwa katika maduka ya uuzaji bidhaa, benki na vituo vya treni.

Hospitali moja inamipango ya kuajiri roboti zaidi kwa miaka 10 ijayo. Baadhi ya wataalamu wamehoji umuhimu wa roboti za kijamii kama vile Pepper.
Kampuni ya softbank, iliyomtengeneza Pepper na kampuni ya Aldebaran wamepata faida kubwa kwa ubunifu huyo haswa kutoka Japan. Roboti hiyo inaurefu wa kina futi nne na inauwezo wa kutambua sauti za binadamu kwa lugha 20 na inauwezo wa kubaini iwapo inazungumza na mwanamume, mwanamke au mtoto.

chanzo :BBC
ROBOTI KUPOKEA WAGENI HOSPITALINI UBELGIJI ROBOTI KUPOKEA WAGENI HOSPITALINI UBELGIJI Reviewed by Elimutehama on 01:41:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.