MAREKANI YACHUNGUZA AJALI YA GARI LINALOJIENDESHA



Mamlaka ya Marekani inachunguza kifo cha kwanza kilichosababishwa na magari yanayojiendesha yenyewe. Dereva wa gari la Tesla alifariki mjini Florida mnamo mwezi Mei baada ya kugongana na Lori. Kinachochunguzwa ni progamu ya Auto Pilot ya Tesla ambayo hubadilisha mistari ya barabara na kujua iwapo kuna trafiki. Katika taarifa,Tesla ilisema kuwa huenda gari hilo la S halikuweza kubaini upande mweupe wa lori hilo dhidi ya mbingu nyeupe iliokuwa ikionekana mbele yake Kampuni hiyo imesema kuwa ajali hiyo ni hasara kubwa. Ajali hiyo ilisababisha kifo cha dereva Joshua Brown mwenye umri wa miaka 40. Dereva wa lori hilo hakujeruhiwa.
MAREKANI YACHUNGUZA AJALI YA GARI LINALOJIENDESHA MAREKANI YACHUNGUZA AJALI YA GARI LINALOJIENDESHA Reviewed by Elimutehama on 03:48:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.