VITUO 34 VYA MRADI WA DART VYAUNGANISHWA NA MKONGO (fibre) WA TTCL



Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura na Mtendaji Mkuu wa DART, Mhandisi Ronald Lwakatare wametembelea mradi wa kuunganisha vituo ya Mabasi ya Mwendokasi (DART) kwenye mtandao wa mawasiliano wa TTCL kupitia njia ya Mkongo ili kiimarisha mifumo ya mawasiliano ndani ya vituo hivyo na DART na UDART.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura na Maafisa kutoka TTCL wakikagua kifaa katika kituo cha Mabasi ya Mwendokasi.

Katika ziara hiyo iliwahusisha wadau wengine kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina,DART, UDART, TTCL, Wakala wa Serikali Mtandao pamoja na Maxmalipo walitembelea vituo vya Kivukoni, Posta ya zamani, Kagera na Jangwani

Akitoa tathimini ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha vituo hivyo, Meneja Mradi wa TTCL, Mhandisi Amossy Itozya amesema kuwa Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) imekamilisha kuunga jumla ya vituo 34 vya DART kwenye mtandao wa TTCL kwa kutumia Mkongo(Fibre).

“Kwa kutumia Mkongo utasaidia kuondokana na changamoto ambazo zilikuwepo awali za kukatika mawasiliano na kuleta usumbufu kwa watumiaji wa huduma ya usafiri. Kwa kutumia Mkongo(fibre) tunauhakika wa kuimarisha mifumo yetu ya ndani na kwenye vituo vya mwendokasi hivyo kuondoa usumbufu kwa wananchi katika kupata huduma” amesema Mhandisi Lwakatare.

chanzo:matukio-michuzi

VITUO 34 VYA MRADI WA DART VYAUNGANISHWA NA MKONGO (fibre) WA TTCL VITUO 34 VYA MRADI WA DART VYAUNGANISHWA NA MKONGO (fibre) WA TTCL Reviewed by Elimutehama on 01:54:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.