HUDUMA YA BURE YA MTANDAO KUTOLEWA KAMPALA NA ENTEBBE.
Serikali ya Uganda imetangaza leo kuwa itatoa huduma ya bure ya intaneti kwenye mji mkuu Kampala na ule wa Entebbe kuanzia siku ya Jumapili.
Waziri wa teknolojia ya habari na mawasiliano Frank Tumwebaze anasema kuwa Uganda huenda ikawa nchi ya kwanza kweye jumuiya ya Afrika Mashariki kuzindua huduma kama hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari aliye kampala, ni kuwa hata hivyo huduma hiyo itakuwa na masharti yake. Kwa mfano itakuwa ikutumiwa tu kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili alfajiri siku za wiki, na kuanzia saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili asubuhi siku za wikendi.
Pia anasema kuwa mitandao kadha itafungwa.
HUDUMA YA BURE YA MTANDAO KUTOLEWA KAMPALA NA ENTEBBE.
Reviewed by Elimutehama
on
05:51:00
Rating:
No comments: