MTOTO WA KWANZA DUNIANI KUTOKA KWA WAZAZI WATATU
Mtoto mmoja wa kiume nchini Mexico kutoka kwa wazazi wenye asili ya Jordan azaliwa akiwa na hali nzuri ya afya baada ya kutoka kwa wazazi watatu.
Mtoto huyo ambaye alizaliwa kupitia mbinu mpya ya kisayansi na wanasayansi wa Marekani alizaliwa miezi mitano iliyopita nchini Mexico.
Wanasayansi kutoka Marekani walitumia mayai ya wazazi watatu kutoka Jordan baada ya mama mzazi kutambulika na ugonjwa wa chembe za urithi ambao ulimfanya kuwa na matatizo ya kuweza kustahimili ujauzito.
Marekani sasa imekubali mbinu hiyo mpya ya kupandikiza mimba ya mayai matatu kwa madhumuni ya uzazi.
MTOTO WA KWANZA DUNIANI KUTOKA KWA WAZAZI WATATU
Reviewed by Elimutehama
on
01:46:00
Rating:
No comments: