WATANZANIA 10 KWENDA KUFANYA KAZI STARTIMES NCHINI CHINA



Washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.

Hatimaye shindano la kusaka vipaji vya sauti lililoandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania limemalizika mwishoni mwa wiki hii kwa watanzania 10 kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu yake yaliyopo jijini Beijing.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.

Naye kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao amebainisha kuwa amefurahi kuona shindano la kusaka vipaji vya sauti limepokewa kwa muitikio mkubwa na watanzania sehemu mbalimbali za nchi.
WATANZANIA 10 KWENDA KUFANYA KAZI STARTIMES NCHINI CHINA WATANZANIA 10 KWENDA KUFANYA KAZI STARTIMES NCHINI CHINA Reviewed by Elimutehama on 00:09:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.