CHINA YARUSHA ROKETI KUBWA ZAIDI



China imerusha roketi yenye uwezo mkubwa zaidi wa kubeba mizigo jana usiku.Roketi kubwa zaidi kuwahi kuundwa katika taifa hilo, roketi iliyopewa jina changzheng no.5 au long March 5.
Roketi hiyo inaonekana "nene" zaidi kuliko roketi nyingine aina ya Changzheng. Roketi hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 25 na kusafiri katika mzingo wa chini wa dunia, ni roketi kubwa zaidi kurushwa ya China.

Roketi hiyo ilirushwa angani kutoka kituo cha shughuli za anga za juu cha Wenchang katika mkoa wa Hainan. Imebeba setilaiti ya kufanya majaribio ambayo imepewa jina Shijian-17.
Long March 5 inaipa Uchina uwezo wa kupeleka angani mitambo na mizigo mizito, kwa mfano mitambo ya kutumiwa kwa ajili ya mawasiliano na vifaa vya kuunda kituo cha anga za juu ambacho taifa hilo linapanga kujenga katika anga za juu. Maelezo ya roketi hiyo yanaashiria ina uwezo wa kubeba tani 25 hadi mzingo wa chini wa dunia (LEO), kilomita kadha juu angani, na tani 14 hadi mzingo wa mbali wa dunia, ambao ni kilomita 36,000 kutoka ardhini.

Long March 5 imo kwenye kitengo sawa na cha roketi yenye nguvu zaidi ya Marekani, roketi ya Delta-IV Heavy. Kampuni za Marekani za SpaceX na Blue Origin zinaunda vyombo vya anga za juu vyenye uwezo wa kusafirisha tani zaidi ya 50 katika mzingo wa chini wa dunia (LEO).
Shirika la anga za juu la Marekani (Nasa) pia linakaribia kufanya safari ya kwanza ya roketi kubwa ambayo wanasema ina uwezo wa kubeba tani 130 hadi LEO.
CHINA YARUSHA ROKETI KUBWA ZAIDI CHINA YARUSHA  ROKETI  KUBWA ZAIDI Reviewed by Elimutehama on 05:35:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.