UFARANSA NI NCHI YA KWANZA DUNIANI KUWA NA MABASI YA KUCHUKUA ABIRIA YASIYOKUWA NA DEREVA



Usafiri wa umma bila malipo nchini.
Manispaa ya Paris wameanzisha matumizi ya mabasi yanayotumia umeme kusafirisha abiria kwa masafa mafupi.Usafirishaji kwa kutumia mabasi hayo unafanyiwa majaribio kwa muda wa miezi 3.Matumizi ya mabasi hayo ya umeme ni katika juhudi za kupunguza uchafuzi wa anga.Mabasi hayo yana kamera maalum, na yanaweza kubeba jumla ya abiria 10. Mabasi huelekeza wenyewe kwa kutumia GPS na stereovision kamera.



Aidha magari hayo pia yanaenda mwendo wa pole pole. Kwa kilomita 20 (maili 12) kwa saa.Kwa kawaida jijini Paris linamsongamano wa magari na uchafuzi wa hewa huongezeka zaidi majira ya baridi.Manispaa ya mji huo ili kupunguza utumizi wa magari ya kibinafsi pia imefanya usafiri wa umma kufanywa bila malipo . Serikali ya Ufaransa ina mipango ya kuongeza mabasi zaidi katika siku zijazo kulingana na mafanikio ya mabasi hayo.
UFARANSA NI NCHI YA KWANZA DUNIANI KUWA NA MABASI YA KUCHUKUA ABIRIA YASIYOKUWA NA DEREVA UFARANSA NI NCHI YA KWANZA DUNIANI KUWA NA MABASI YA KUCHUKUA ABIRIA YASIYOKUWA NA DEREVA Reviewed by Elimutehama on 01:42:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.