GOOGLE YASANIFU SOFTWARE MPYA KUWASAIDIA WAZAZI KUWADHIBITI WATOTO KUTUMIA SIMU ZA MKONONI
Je, una wasiwasi kwamba watoto wako wanachezea simu za mkononi kwa muda mrefu kupita kiasi au kusoma habari zisizofaa watoto? Kampuni ya Google imetangaza kuwa imesanifu software mpya iitwayo Family Link, ambayo inaweza kuwasaidia wazazi kudhibiti watoto wenye umri chini ya miaka 13 kutumia simu za mkononi au kompyuta aina ya tablet.
Software hii inawaruhusu watoto kutumia huduma za Google zikiwemo barua pepe, ramani na software ya kutembelea mtandao wa Internet, lakini wazazi wanaweza kuamua muda wao wa kutumia software mbalimbali, na kuwazuia wasitembelee baadhi ya tovuti.
Kampuni ya Google ilitoa toleo la majaribio la software hii, hivi sasa linaweza kutumiwa kwenye simu na tablets zenye mfumo wa Android. Toleo rasmi litatolewa baadaye mwaka huu, na toleo kwa simu za iPhone na iPad bado linasanifiwa.
Uchunguzi uliofanyika mwaka jana unaonesha kuwa kwa wastani watoto wa Marekani wanapata simu zao za mkononi katika umri wa miaka 10.3, asilimia 39 ya watoto wana akaunti zao za tovuti za SNS katika umri wa miaka 11.4, na asilimia 84 ya watoto wenye umri kati ya miaka 6 hadi 12 wanacheza tablets mara moja au zaidi kwa wiki.
GOOGLE YASANIFU SOFTWARE MPYA KUWASAIDIA WAZAZI KUWADHIBITI WATOTO KUTUMIA SIMU ZA MKONONI
Reviewed by Elimutehama
on
03:29:00
Rating:
No comments: