TUNAWEZA SEMA CYBORGS KAZINI: WAFANYAKAZI WA KISWIDISHI KUPANDIKIZWA MICROCHIPS MWILINI.



Sindano hudungwa katika kati ya kidole gumba na kidole cha shahada. Kisha, microchip hudungwa au huwekwa katika mkono wa mfanyakazi kuundwa kwa "Cyborg" . mchakato huchukua sekunde chache, na mara nyingi zaidi hakuna kelele na vigumu kuona tone la damu.

Katika Epicenter taasisi inayohusiana na teknolojia swedeni (Swedish startup hub Epicenter) . kampuni inatoa wafanyakazi wake kupandikizwa microchips ukubwa wa punje ya nafaka ya mchele na kwamba inafanyakazi kama kadi (swipe cards): ya kufungua milango, kuendesha Printers, au kununua vitu kwa kutumia mkono.Sindano hizo zimekuwa maarufu kwa wafanyakazi katika kitovu cha kazi Epicenter kwa wale tayari kupata huduma ya kupandikizwa mwilini.

"Faida kubwa nadhani ni urahisi," alisema Patrick Mesterton, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Epicenter . Kama mfano, yeye kufungua mlango kwa pungia tu karibu yake. " kimsingi inapunguza nafasi ya kuwa na mambo mengi, vifaa vingi vya mawasiliano, iwe ni credit card au funguo."



Epicenter ambapo ni nyumbani kwa makampuni zaidi ya 100 na baadhi ya wafanyakazi 2,000, ilianza kupandikiza wafanyakazi microchips katika mwezi Januari 2015. Sasa, ina wafanyakazi 150 ambao wamepandikizwa microchips au kuwa nazo mwilini. Upandikizaji huo mdogo kutumia teknolojia ya NFC(Near Field Communication technology), sawa kabisa kama zinazotumika katika kadi za fedha/malipo(credit cards) au malipo ya simu za mkononi.



Ben Libberton, ni microbiologist katika Taasisi ya Karolinska ya Stockholm nchini swedeni, anasema wadukuzi( hackers) watataka kupata taarifa kubwa kutoka kwa microchips iliyoingia. Na hii kimaadili na madhara yatakuwa makubwa zaidi pindi matumizi zaidi microchips kuwa.

"Kwamba kuna uwezekano wa kupata Data kutoka Chip iliyoingia katika mwili wako ni nyingi tofauti na data unaweza kupata kutoka simujanja(smartphone)," anasema. "kwa mfano unaweza kupata data kuhusu afya yako, unaweza kupata data kuhusu mienendo yako, mara ngapi wewe unaenda kazini, kwa muda gani wewe hufanya kazi, kama wewe kuchukua mapumziko au hata kwenda chooni na vitu kama hivyo."

Libberton alisema kwamba kama data zinakusanywa, swali kubwa bado linabaki nini kitakachotokea kwa hilo, nani anayetumia , na kwa madhumuni gani.

Hadi sasa, kikundi cha Epicenter cyborgs hawaonekani kuwa na wasiwasi.
TUNAWEZA SEMA CYBORGS KAZINI: WAFANYAKAZI WA KISWIDISHI KUPANDIKIZWA MICROCHIPS MWILINI. TUNAWEZA SEMA CYBORGS KAZINI: WAFANYAKAZI WA KISWIDISHI KUPANDIKIZWA  MICROCHIPS MWILINI. Reviewed by Elimutehama on 03:31:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.