WHATSAPP KUZINDUA HUDUMA YA KUTUMA NA KUPOKEA FEDHA , KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6.
Hii itakuwa ni moja ya huduma ya fedha kwa programu(app) ya kutuma ujumbe kwa kampuni kubwa duniani . India ndio itakafanyiwa majaribio katika kipindi cha miezi 6 ijayo, india inawatumiaji wa Whatsapp wakubwa katika soko, ambao ni zaidi ya milioni 200,ni inchi inayopiga hatua katika uchumi wa kijiditali.
Ni wazi kama kipengele hiki cha fedha kisaidia nchi nyingi, lakini ni kawaida kwa Facebook kampuni inayomiliki Whatsapp kutoa huduma mpya kwa majaribio katika baadhi ya nchi kabla ya kuwaleta watu dunia kote.
Whatsapp si programu ya kwanza ya kutuma ujumbe kujitosa katika soko la malipo au fedha ya digitali. Katika mwaka 2014, programu ya ujumbe ya WeChat ya China ilizindua huduma zake za fedha , WeChat Pay katika nchi ya China, inawatumiaji zaidi ya milioni 800 tangu kusajiliwa .
WHATSAPP KUZINDUA HUDUMA YA KUTUMA NA KUPOKEA FEDHA , KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6.
Reviewed by Elimutehama
on
02:03:00
Rating:
No comments: