TWITTER KUFANYIWA MABADILIKO ILI KUWAVUTIA WATUMIAJI

Mtandao wa Twitter unafanyia marekebisho sheria zake ili kuwarahasishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza.

Wanachama wa mtandao hao sasa wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo, zikiwemo picha na video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili kuandika.

Twitter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao. Mwanzilishi mwenza wa Twitter na mkurugenzi mkuu Jack Dorsey, aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa wakati watu wanapoutumia unaonekana kuwa ulio na maana.

Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake.

Licha ya mtandao huo kutumiwa sana katika masuala yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia. Brian Blau, ambaye ni mchambuzi kutoka shirika la Gartner, anasema matatizo yanaoikumba Twitter kuwapata watumiaji wapya hayawezi kutatuliwa na mabadiliko hayo.

Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao. Anaendelea kusema kuwa bado Twitter haijalishughulikia hilo.

chanzo bbc.
TWITTER KUFANYIWA MABADILIKO ILI KUWAVUTIA WATUMIAJI TWITTER KUFANYIWA MABADILIKO ILI KUWAVUTIA  WATUMIAJI Reviewed by Elimutehama on 05:19:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.