VODACOM TANZANIA YAZINDUA MTANDAO WA 4G WENYE KASI ZAIDI
Kampuni ya Vodacom Tanzania Alhamis hii ilizindua rasmi mtandao wa 4G utakaowawesha wateja wake wa jijini Dar es Salaam kupata internet yenye kasi zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akizungumza kwenye uzinduzi huo
Uzinduzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akiongea kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema kuwa spidi ya mtandao wa 4G wa Vodacom haina tofauti na ile inayopatikana kwenye nchi zilizoendelea.
Alisema kuwa mtandao huo utatumika kama chachu ya maendeleo kwenye sekta nyingi nchini.
“4G kwetu sio teknolojia, 4G kwetu ni kiwezeshaji, ni kiwezeshaji kwa serikali, kiwezeshaji kwa biashara, ni kiwezeshaji kwa watumiaji wetu,” alisema. “Inachofanya inafungua fursa mpya, uwezekano mpya,” aliongeza.
Kwa upande wake Rosalynn Mworia ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, amewataka wateja wa Vodacom kwenda kwenye maduka yao ili kuweza kubadilishiwa laini zao za simu na kupewa mpya zilizowezeshwa na teknolojia ya 4G.
“Kwa kifupi ni kwamba mteja ataweza kupata internet ambayo ina spidi kuliko zote na ataweza kudownload kama ni movie akaziangalia live bila buffering,” alisema.
Bi Mworia aliongeza kuwa pamoja na mteja wa Vodacom kupata laini ya 4G, bado atapewa vifurushi vya bure vya internet zikiwemo GB 4 atakazoweza kuzitumia ndani ya masaa 48. “Lakini pia kwa mwaka mzima, kila anaweka vocha na kujiunga na kifurushi, anapata GB 1 ya nyongeza ambayo ina validity ya mwaka mzima
Wanamuziki wa kundi la Mafikizolo wakitumbuiza

Reviewed by Elimutehama
on
04:35:00
Rating:
No comments: