CHINA YARUSHA KWA MAFANIKIO CHOMBO CHA ANGA YA JUU KINACHOBEBA BINADAMU SHENZHOU-11



China imerusha kwa mafanikio chombo cha anga ya juu kinachobeba binadamu. Majukumu ya chombo hicho kinachojulikana kama Shenzhou-11 ni kupeleka wanaanga na vifaa kwenye maabara yaliyo anga ya juu Tiangong-2, kuifanyia majaribio teknolojia za kuunganisha vyombo vya anga ya juu na kurudisha vyombo hivyo duniani, kuungana na maabara ya Tiangong-2 ambako upimaji wa afya ya wanaanga, tathmini ya kazi zao zitafanyika, na majaribio ya matibabu ya anga na sayansi ya anga yatafanyika.



Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini India, ametoa pongezi akisema hatua hiyo inaonesha kuwa mradi wa China wa kuwaasfirisha binadamu kwenye anga ya juu umepata maendeleo makubwa.
CHINA YARUSHA KWA MAFANIKIO CHOMBO CHA ANGA YA JUU KINACHOBEBA BINADAMU SHENZHOU-11 CHINA YARUSHA KWA MAFANIKIO CHOMBO CHA ANGA YA JUU KINACHOBEBA BINADAMU SHENZHOU-11 Reviewed by Elimutehama on 03:32:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.