PROGRAMU MPYA YA MICROSOFT INAYOFAHAMU MAZUNGUMZO KAMA VILE BINADAMU



Microsoft inadai kuwa imeumba teknolojia ambayo, kwa mara ya kwanza kabisa, inaweza kuelewa mazungumzo ya binadamu kama vile mtu anavyoelewa . Katika mada iliyochapishwa Oktoba 18, watafiti kutoka Microsoft katika timu ya intelegensia isiyo halisi(Artificial Intelligence) au AI na Utafiti imetoa taarifa kwamba kwa kutumia AI wameunda mfumo wa mazungumzo wa kutambua na ulifanya sawa au makosa machache ya kitaaluma.

Kwa mujibu wa timu ya teknolojia inauwezo wa kufanya kosa katika neno kwa kiwango cha (word error rate (WER) ) asilimia ya 5.9,wameweza kupunguza ukubwa kutoka asilimia 6.3 ambapo timu ilikuwa imefikia mwezi uliopita tu.

Xuedong Huang, mkuu wa kampuni katika kitengo cha wanasayansi hao alithibitisha matokeo akisema "Tumeweza kufikia usawa wa binadamu, haya ni mafanikio ya kihistoria." Matokeo si tu yamekuwa mazuri lakini yamezidi lengo walilojiwekea kwa mwisho wa mwaka, lakini hili litakuwa na matarajio ya wengi katika sekta hiyo.

Harry Shum, makamu wa rais na mtendaji ambaye anaongoza kundi la Microsoft Artificial Intelligence na Utafiti alisema: "Hata miaka mitano iliyopita, mimi sikuwa na mawazo tunaweza kuwa na mafanikio haya. Mimi nilikuwa na mawazo haitawezekana, "

JE, WW UNAONA WANASAYANSI WATAFIKIA UWEZO WAKUWA SAWA NA BINADAMU : TOA MAONI YAKO.
PROGRAMU MPYA YA MICROSOFT INAYOFAHAMU MAZUNGUMZO KAMA VILE BINADAMU PROGRAMU MPYA YA MICROSOFT INAYOFAHAMU MAZUNGUMZO KAMA VILE BINADAMU Reviewed by Elimutehama on 04:23:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.