GOOGLE WATAMBULISHA SIMU MPYA AINA GOOGLE PIXEL NA PIXEL XL KIASI FULANI ITAKABILIANA NA VUMBI SUGU.



5-inch Pixel na 5.5-inch Pixel XL zitafika sokoni katika maduka na mitandaoni Oktoba 20. Google imekuja na aina mbili za simu zenye uwezo wa kuhifadhi data zako , 32GB na 128GB, na Google Pixel la chaguo dogo la kuhifadhi itakugharimu wewe kiasi cha dola za kimarekani $ 649,au pound za uingereza £ 599. Wakati huo huo Google Pixel XL kwa bei ambayo ni $769 (32GB); $869 (128GB).

Pixel na Pixel XL, ambayo Google ilizindua Jumanne, itatoa ulinzi dhidi ya baadhi mambo yatokanayo na unyevu na vumbi, shukrani kwa cheti cha IP53(International Protection Rating) . Tume ya kimataifa ya ulinzi wa vifaaa , zaidi inajulikana kama IP rating, ni ya kiwango ambacho kimependekezwa kwa tume ya kimataifa ya International Electrotechnical ambayo inajulikana kama "mfumo kwa kuainisha madaraja ya ulinzi unatolewa katika hakikisho la vifaa vya umeme."

katika kanuni namba 5 inaonyesha kwamba kifaa " kina ulinzi japokuwa mdogo kutoka katika kukabiliana na vumbi linalodhuru," wakati kanuni namba 2 inawakilisha ulinzi dhidi ya vimiminika mtiririko kama maji yatakayorushwa kama spray katika kifaa. Katika jambo hilo, "maji yatakapo anguka katika pembe yoyote hadi nyuzi 60 kutoka wima hayatakuwa na nguvu na madhara" kwenye simu za Google.

Hii kimsingi ina maana ni kwamba uko salama kwa matumizi moja ya simu hizi katika mvua, lakini pengine ni bora kuiacha karibu na taulo yako wakati wewe ukwenda kuoga au kuogelea.



Moja ya sifa kubwa mpya kwa Pixel ni ushirikishwaji wa usaidizi wa Google yenyewe(Google Assistant) . Pixel na Pixel XL sasa kuwa na mfumo mpya-au wa kipekee kuangalia usaidizi , ambao una lengo la kukupa wewe binafsi mambo yako mwenyewe ya Google katika simu yako.
GOOGLE WATAMBULISHA SIMU MPYA AINA GOOGLE PIXEL NA PIXEL XL KIASI FULANI ITAKABILIANA NA VUMBI SUGU. GOOGLE WATAMBULISHA SIMU MPYA AINA GOOGLE PIXEL NA PIXEL XL KIASI FULANI ITAKABILIANA NA VUMBI SUGU. Reviewed by Elimutehama on 04:06:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.