JOHN GLENN :MWANAANGA WA KWANZA KUFIKA ANGA ZA JUU AFARIKI
John Glenn ni mwanaanga wa kwanza kutoka Marekani kuwahi kufanya safari mbili angani kwa mafanikio . Glenn amefariki siku ya Alhamis akiwa na umri wa miaka 95 .
Glenn alivutia watu wengi kutoka pande zote za dunia hasa baada ya mafanikio yake. Alihudumia jeshi la Marekani,shirika la NASA na pia kama seneti wa Marekani.
Mnamo mwaka 1959 alichaguliwa katika kundi la 'Original Seven ' kama wanaanga wa kwanza kufanya safari ya mbali angani. Glenn alifariki akiwa katika hospitali ya James Cancer ingawaje sababu kamili ya kifo chake bado haijulikani.
JOHN GLENN :MWANAANGA WA KWANZA KUFIKA ANGA ZA JUU AFARIKI
Reviewed by Elimutehama
on
04:44:00
Rating:
No comments: