FACEBOOK YAKIRI MAKOSA YA KUIBIWA KWA DATA YATANGAZA HATUA MPYA KULINDA DATA ZA WATUMIAJI



Mkurungenzi mkuu mtendaji wa kampuni ya Facebook Bw. Mark Zuckerberg alipozungumzia tukio la kuibiwa kwa data za watumiaji alisema kampuni yake imefanya makosa katika kuhifadhi data za watumiaji, na ameahidi kuwa kampuni yake itachukua hatua kutatua tatizo hilo.

Facebook imetangaza mabadiliko kadhaa kuwapa watumiaji udhibiti zaidi wa taarifa zao, baada ya kashfa kubwa ya data ilioigharimu zaidi ya dola bilioni 100. Marekebisho hayo yanafuatia ukosoaji mkubwa dhidi ya Facebook. Bw. Zuckerberg amesema kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba mtafiti wa Chuo Kikuu cha Cambridge amepata data za watumiaji wa Facebook na kuzipa kampuni ya uchambuzi wa data iitwayo Cambridge Analytica.

Amesema Facebook ina wajibu wa kuhifadhi data za watumiaji, imefanya makosa, na inatakiwa kufanya kazi nyingi mapema. "Hivyo, mbali na tangazo la Mark wiki iliyopita -- kuhusu kukabiliana na ukiukaji wa jukwaa la Facebook, kuimarisha sera zetu, na kuwarahisishia watu kuondoa uwezo wa App kutumia data zako-- tunachukuwa hatua za ziada katika wiki zijazo kuwapa watu udhibiti zaidi wa faragha zao."

"Wiki iliyopita imeonyesha ni kazi kiasi gani tunatakiwa kufanya kutekeleza sera zetu, na kuwasadia watu kuelewa namna Facebook inavyofanya kazi, na fursa za kuchagua data walizonazo kuhusu taarifa zao," Erin Egan, makamu wa rais na mkuu anayehusika na faragha, na Ashlie Beringer, makamu wa rais na naibu wakili mkuu wa Facebook, waliandika katika chapisho la blogi.

Hivi sasa tovuti nyingi zinaidhinisha hadhi ya watumiaji kwa akaunti za Facebook. Kampuni ya Facebook imetoa taarifa ikisema itachukua hatua kuzuia kampuni nyingine kupata data za watumiaji bila kuidhinishwa na Facebook. Hivi karibuni vyombo vingi vya habari vimesema data za watumiaji milioni 50 zimepatikana na kutumiwa na kampuni ya Cambridge Analytica, na kampuni ya Facebook ilitambua jambo hili, lakini haikutangaza kwa wakati.

Kampuni hiyo ilikumbana na malalamiko kutoka kona mbalimbali za dunia baada ya mfichuaji kubainisha Machi 17, kwamba data kutoka watumiaji milioni 50 zilichotwa isivyo sahihi kuwalenga wapigakura nchini Uingereza na Marekani katika chaguzi zilizokuwa na ushindani mkubwa.

FACEBOOK YAKIRI MAKOSA YA KUIBIWA KWA DATA YATANGAZA HATUA MPYA KULINDA DATA ZA WATUMIAJI FACEBOOK YAKIRI MAKOSA YA KUIBIWA KWA DATA YATANGAZA HATUA MPYA KULINDA DATA ZA WATUMIAJI Reviewed by Elimutehama on 02:49:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.