MAGARI YA DIZELI KUPIGWA MARUFUKU KUANZIA MWAKA 2025
Mkutano wa C40 unaohusisha viongozi wa manispaa mbalimbali za miji nchini Mexico ulifanyika katika mji mkuu wa Mexico City kujadili suala la uchafuzi wa mazingira. Katika mkutano huo, viongozi wa manispaa za miji ya kimataifa kama vile Paris Ufaransa, Madrid Uhispania na Athens Ugiriki pia walihudhuria.
Viongozi hao walichukuwa uamuzi wa kuweka marufuku ya matumizi ya magari yanayotumia mafuta ya dizeli kuanzia mwaka 2025 kama mojawapo ya hatua za kupunguza uchafuzi wa mazingira mijini.
Meya wa manispaa ya mji wa Paris Anne Hidalgo, meya wa Mexico City Miguel Angel Marcera, meya wa Madrid Manuela Carmena pamoja na meya wa Athens Giorgos Camins walitia saini mkataba huo wa makubaliano wa kuzuia magari ya dizeli na kuruhusu matumizi ya magari ya nishati za umeme na gesi.
Viongozi hao pia waliarifu kuanzisha mpango wa kushawishi wakaazi wa miji kutumia baiskeli au kutembea kwa miguu ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Mnamo mwezi Aprili, bunge la Uholanzi liliwahi kuidhinisha kanuni ya marufuku dhidi ya matumizi ya magari ya dizeli kuanzia mwaka 2025.
Viongozi wa Ujerumani nao waliwahi kutangaza mpango wa kusitisha mauzo ya magari ya dizeli kuanzia mwaka 2030.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HILI .
MAGARI YA DIZELI KUPIGWA MARUFUKU KUANZIA MWAKA 2025
Reviewed by Elimutehama
on
02:09:00
Rating:
No comments: