MATAIFA YA ULAYA KUTUMA CHOMBO SAYARI YA MARS
Mawaziri wa utafiti kutoka bara Ulaya wanaokutana mjini Lucerne, Uswizi wamesisitiza kwamba mpango wa kutuma chombo maalum kinachoweza kusafiri kwenye sayari ya Mars mwaka 2021 bado utaendelea.Wameahidi kutoa jumla ya euro €436m ambazo zinahitajika kufanikisha mpango huo.
Mradi huo umechelewa kiasi na unagharimu pesa zaidi kuliko ilivyotarajiwa, jambo lililoibua wasiwasi kwamba mataifa wanachama wa Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA) huenda wakaufuta mpango huo.
Lakini mawaziri hao wamesema bado wamejitolea kuufanikisha.Wamesema ushiriki wa nchi za Ulaya katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) unafaa kuendelea hadi angalau 2024, na kuiwezesha ESA kufikia washirika wengine katika kituo hicho kinachoizunguka dunia - Marekani, Urusi, Japan na Canada.
Hilo litatoa fursa mpya kwa wana anga kutoka Ulaya kutembelea kituo hicho.Kwenye mkutano huo wa mawaziri, imetangazwa kwamba Mwitaliano Luca Parmitano amependekezwa kuzuru kituo hicho 2019.
Mwitaliano Luca Parmitano
Mkutano huo wa mawaziri uliitishwa kujadili sera, miradi na ufadhili wa ESA kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano ijayo.Mawaziri hao kutoka nchi 22 waliidhinisha kutumiwa kwa €10.3bn.
chanzo:bbc
MATAIFA YA ULAYA KUTUMA CHOMBO SAYARI YA MARS
Reviewed by Elimutehama
on
02:20:00
Rating:
No comments: