VIFAA VYA ELEKTRONIKI VYA BINAFSI KUTORUHUSIWA KATIKA NDEGE ZINAZOELEKEA MAREKANI



Abiri wanaomiliki vifaa vya elektroniki wanazuiwa na Marekani kusafiri na vifaa hivyo katika safari za ndege za kuelekea Marekani. Vifaa hivyo vitashirikisha Laptopu, kamera za tabiti [tablet], vifaa vya kuchezesha kanda za video pamoja na zile za michezo ya kielektroniki lakini simu hazikutajwa. Marekani inapiga marufuku vifaa vya kielektroniki kuingia katika ndege kutoka mataifa manane ya mashariki ya kati na Afrika Kaskazini.

Kwanzia hii leo siku ya Jumanne shirika la ndege la Royal Jordanian Airlines litawazuia abiria wake kusafiri na vifaa vya elektroniki kama vipakatilishi,iPads,kamera na vinginevyo katika safari za ndege za kuelekea Marekani.Shirika la ndege la Jordan lilisambaza ujumbe huo kupitia akaunti ya mtandao wa Twitter .

Katibu wa usalama wa nchi wa Marekani John Kelly afahamisha kuwa aliwapigia simu wabunge kuhusu sheria hiyo mpya ya usalama katika idara ya anga na kukubali kutumia mbinu hiyo mpya .Hata hivyo mtaalamu wa usalama katika shirika la ndege la Jordan alisema kuwa marufuku hiyo mpya pia itazua masuala mengine ya kiusalama .
VIFAA VYA ELEKTRONIKI VYA BINAFSI KUTORUHUSIWA KATIKA NDEGE ZINAZOELEKEA MAREKANI VIFAA VYA ELEKTRONIKI VYA BINAFSI KUTORUHUSIWA KATIKA NDEGE ZINAZOELEKEA MAREKANI Reviewed by Elimutehama on 04:21:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.