TRENI YA KWANZA DUNIANI INAYONING'INIA CHINI YA RELI YA JUU YAFANYA SAFARI ZA MAJARIBIO NCHINI CHINA
Treni ya kwanza duniani inayotumia betri za Li-ion inayoning'inia chini ya reli ya juu imefanya safari za majaribio mjini Chengdu China. Treni hiyo inaendeshwa katika reli yenye umbo la U katika eneo la uendelezaji wa uchumi na teknolojia la uwanja wa ndege wa Shuangliu mjini Chengdu. Reli hii ya majaribio inaundwa na majengo na vifaa mbalimbali vikiwemo stesheni, reli mbili, treni na gereji, inaweza kupima uwezo wa treni kwenye njia inayonyooka, inayopinda na mteremko. China ina haki kamili ya kumiliki mfumo huu mpya wa kisasa wa usafiri. Zhai Wanming, mkuu wa ubunifu wa mradi huu amesema treni hiyo aina mpya inatumia gharama ndogo katika utengenezaji na rafiki wa mazingira ukilinganisha na treni za umeme na treni za mafuta.
TRENI YA KWANZA DUNIANI INAYONING'INIA CHINI YA RELI YA JUU YAFANYA SAFARI ZA MAJARIBIO NCHINI CHINA
Reviewed by Elimutehama
on
05:43:00
Rating:
No comments: