WASHINDI APPSAFRICA INNOVATION AWARD WATANGAZWA



Washindi kumi wa AppsAfrica.com Innovation Awards 2016 walitangazwa katika moja ya sherehere za tuzo za wadau wa teknolojia na simu Afrika mjini Cape Town, Afrika Kusini.

Tuzo zinahusu application za simu ziliungwa mkono na Opera Software, The Mobi Hunter, Uber, Shule Direct, Mobile Monday South Africa and The Mobile Ecosystem Forum (MEF) ni sherehe bora katika simu na teknolojia kutoka Afrika na kuwavutia zaidi ya washiriki 200 kutoka nchi 25. Mwaka huu tuzo ziliwavutia zaidi ya washiriki 200 kutoka nchi 25, na washindi walitokea Afrika Kusini, Nigeria, Zambia, Kenya, Uganda na Tanzania.

Washindi wa mwaka 2016 wa Appsafrica.com Innovation Awards:

Disruptive Innovation Award
Domestly (South Africa)

Social and Messaging Award
Vula Mobile (South Africa)

Best African App Award
Sliide Airtime (Nigeria)

Enterprise Solution Award
Flutterwave (Nigeria)

News & Entertainment Award
Battabox (Nigeria)

Educational Award
Mwabu (Zambia)

Fintech Award
BitPesa (Kenya)

Social Impact Award
Ask without Shame (Uganda)

Brand On Mobile Award
Mobi Hunter (South Africa)

Women In Tech Award
Faraja Nyalandu – Shule Direct (Tanzania)

"Dhamira yetu katika Appsafrica.com ni kukuza na kuheshimu uvumbuzi wa ajabu katika mazingira ya simu na teknolojia barani Afrika. Tulikuwa na washiriki mbalimbali kutoka nchi 25 na wote washindi waliofika fainali walitakiwa waoneshe ushahidi wa jinsi teknolojia inavyoweza kutumika kusaidia mfano biashara, kuwawezesha watu na kuleta athari chanya katika jamii barani Africa kwa pamoja” alisema Andrew Fassnidge mwanzilishi wa Appsafrica.com.
WASHINDI APPSAFRICA INNOVATION AWARD WATANGAZWA WASHINDI APPSAFRICA INNOVATION AWARD WATANGAZWA Reviewed by Elimutehama on 05:39:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.