MIWANI JANJA YA GOOGLE IMERUDI
Google imefanya marekebisho ya toleo jipya ya miwani zake janja kwa ajili ya biashara, baada ya zaidi ya miaka miwili toleo la awali la bidhaa zake kufutwa. Kampuni hiyo imesema miwani toleo jipya imeboreshwa katika maisha ya betri kuishi muda mrefu na muonekano mzuri zaidi kuliko kabla.Hata hivyo, bado inafanana na mfano wa awali,miwani hiyo inayojulikana kama Google Glass Enterprise Edition(GE).
Katika chapisho la blogu inayozungumzia toleo jipya, Jay Kothari, muongozaji mradi kwenye Google Glass, alibainisha matukio mengi ya matumizi ya miwani mahali pa kazi, ambapo Google Glass tayari imesaidia.
"GE ilikuwa ni moja ya biashara ilionyesha faida mahali pa kazi," Kothari aliandika, akiongezea kuwa kuna makampuni zaidi ya 50 hutumia miwani, ikiwa ni pamoja na Boeing, Volkswagen, DHL na wengine wengi. "Kulingana na maoni mazuri tuliyopokea kutoka kwa wateja hawa katika programu maalum ambayo tumekuwa tukiendesha kwa miaka miwili iliyopita, sasa tunafanya Toleo la Glass Enterprise linapatikana kwa ajili ya biashara zaidi kupitia mtandao wetu wa washirika."
Toleo la hivi karibuni la miwani liloboreshwa, ikiwa ni pamoja na marekebisho katika kamera. Sasa ina kamera ya megapixel 8, kutoka kwa megapixels 5. Pia itakuwa na betri yenye maisha ya muda mrefu, processor bora, kiashiria cha kurekodi video na kasi ya Wi-Fi.
MIWANI JANJA YA GOOGLE IMERUDI
Reviewed by Elimutehama
on
03:31:00
Rating:
No comments: