YAHOO: WATUMIAJI BILIONI 1 WAMEATHIRIWA NA WAVAMIZI WA MITANDAO



Kampuni ya Intaneti ya Yahoo inasema wavamizi wa mitandao waliiba data za zaidi ya ya watumiaji wake bilioni moja. Tukio hilo linaaminika kufanyika mnano mwaka 2013.
Katika taarifa yake, Yahoo inasema uvamizi huo wa taarifa muhimu ni tofauti na ule ulioripotiwa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo wavamizi hao waliiba taarifa kutoka kwenye akaunti mbalimbali za watumiaji zaidi ya milioni mia tano. Imeongeza kuwa data zilizoibiwa zinajumuisha majina, anuani, namba za simu,tarehe za kuzaliwa pamoja na nywila (namba za siri).
Lakini kadi za malipo sambamba na akaunti za benki hazikuingiliwa.
YAHOO: WATUMIAJI BILIONI 1 WAMEATHIRIWA NA WAVAMIZI WA MITANDAO YAHOO: WATUMIAJI BILIONI 1 WAMEATHIRIWA NA WAVAMIZI WA MITANDAO Reviewed by Elimutehama on 22:49:00 Rating: 5

No comments:

WASILIANA NASI KUPITIA

Barua pepe/Email:123shadhili@gmail.com
copyright@2016. Theme images by enot-poloskun. Powered by Blogger.