AFISA POLISI ROBOTI YA KWANZA YAFANYA KAZI DUBAI
Polisi nchini Dubai wamezindua afisa roboti ya kwanza itakayo piga doria katika majumba ya kibiashara na maeneo ya kivutio kwa watalii.
Watu wataweza kuripoti uhalifu, kulipa faini na kupata taarifa kwa kugusa kompyuta iliopo kifuani mwa roboti hiyo. Taarifa inayokusunywa na roboti hiyo itasambazwa kwa maafisa wa usafiri na trafiki. Serikali inasema inalenga kuwa 25% ya kikosi chake kiwe ni cha roboti kufikia 2030 lakini roboti hizo haziwezi kuichukua nafasi ya binaadamu.
"Nafasi za maafisa wa polisi hazitochukuliwa na mashine hii," amesema Brigedia Khalid Al Razooqi, mkurugenzi mkuu wa huduma za kisasa kielektroniki katika idara ya polisi Dubai.
"Lakini kutokana na kuongezeka idadi ya watu Dubai tunataka tuwahamishe maafisa wa polisi ili wafanye kazi katika maeno yanayostahili na waweze kushughulikia kikamilifu kuimarisha usalama mjini".
Roboti inayozungumza lugha tofuati
"Watu wengi hufika katika vituo vya polisi au maeneo ya kuwahudumia wateja, lakini kwa chombo hiki tunaweza kuufikia umma kila siku ya wiki." "Roboti inaweza kuwalinda watu dhidi ya uhalifu kwasababu inaweza kutangaza kinachotokea haraka moja kwa moja hadi katika kituo chetu kikuu cha usimamizi."
Kwa sasa inaweza kuzungumza lugha ya kiarabu na kiingreza, lakini kuna mipango ya kuongeza Kirusi, Kichina, Kifaransa na hata Ki Hispania katika rekodi yake ya lugha.
Huenda roboti ya pili ikaanza kupiga doria mwaka ujao iwapo ufadhili utapatikana, serikali ya Dubai imesema.
chanzo:bbc
AFISA POLISI ROBOTI YA KWANZA YAFANYA KAZI DUBAI
Reviewed by Elimutehama
on
05:07:00
Rating:
No comments: