KIJANA ALIYEUNDA SETILAITI NDOGO ZAIDI INDIA
Kijana mmoja nchini India ameunda kile kinachotajwa kuwa setilaiti ndogo zaidi ambayo itawekwa kwenye mzingo wa dunia katika kituo cha shirika la safari za anga za juu la Marekani Nasa mwezi Juni.
Kifaa hicho cha Rifath Shaarook cha uzito wa gramu 64, kilichaguliwa kama mshindi wa shindano lililodhaminiwa na Nasa. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 anasema kuwa wajibu ni kuoyesha uwezo wa chapa ya 3-D. Rifath aliviambia vyombo vya habari kuwa kifaa hicho kitafanya safari ya saa nne.
Wakati huo setilaiti hiyo itasafiri kwa muda wa dakika 12 katika mazingira sawa na ya angani,. "Tuliitengeneza kutoka mwanzo," alisema. Satellite hiyo imepewa jina KalamSat, baada ya jina la rais wa zamani wa India Abdul Kalam, ambaye ni mwanzishi wa miradi ya anga za juu ya nchi hiyo.
Mradi huo ulichaguliwa kutoka shindano kwa jina Cubes in Space, lililoandaliwa na NASA pamoja na kampuni ya elimu ya idoodle.
Chanzo :BBC
KIJANA ALIYEUNDA SETILAITI NDOGO ZAIDI INDIA
Reviewed by Elimutehama
on
09:35:00
Rating:
No comments: